Fountain Gate Academy pamoja na Fountain Gate Sports Academy zimeingia makubaliano muhimu na timu ya Jeshi la Kulinda Uchumi (JKU) Zanzibar. Makubaliano haya yanajikita katika maendeleo ya michezo na kuinua vipaji vya vijana kutoka Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Makubaliano haya yanajumuisha:
- Uzinduzi wa jezi mpya ya JKU yenye nembo ya Fountain Gate Schools kama mdhamini rasmi.
- Fountain Gate kuisaidia Timu ya JKU kuanzisha na kuendeleza timu ya wanawake itakayoshiriki katika Ligi Kuu, hii ni kutokana na uzoefu wa Fountain Gate katika soka la wanawake nchini.
- Fountain Gate kutoa nafasi kwa vijana kutoka Zanzibar kucheza mpira katika bara na visiwa, hivyo kuwawezesha kukuza vipaji vyao na kupata fursa za kimataifa.
Makubaliano haya ni hatua muhimu katika kuboresha michezo Zanzibar na kuhakikisha vipaji vinapata fursa sahihi za maendeleo.
Aidha, Mkurugenzi wa Taasisi ya Fountain Gate, Ndg. Japhet Makau, ameonesha nia ya kufungua shule katika kisiwa cha Zanzibar siku zijazo.